Na: Frank Shija – Idara ya Habari –MAELEZO, Singida Halmashauri zote nchini zimetatikiwa kuwa na mkakati wa mawasiliano utakaotumikakufikisha taarifa za utekelezaji wa sshughuli za maendeleo kwa wananchi. Wito huo umetolewa leo Wilayani Mkalama mkoani Singida na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bibi. Zainabu Kawawa wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea changamoto
Na: Frank Shija – Idara ya Habari –MAELEZO, Singida
Halmashauri zote nchini zimetatikiwa kuwa na mkakati wa mawasiliano utakaotumikakufikisha taarifa za utekelezaji wa sshughuli za maendeleo kwa wananchi.
Wito huo umetolewa leo Wilayani Mkalama mkoani Singida na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bibi. Zainabu Kawawa wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea changamoto zinazowakabili Maafisa Habari wa Mikoa ya Kanda ya Kati inayohusisha mikoa ya Tabora, Singida na Dodoma.
Zamaradi amesema kuwa Halmashauri zinaowajibu wa kuajiri na kuwajengea uwezo Maafisa Habari ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuhabarisha jamii juu ya masuala ya maendeleo yanayofanywa na Serikali katika maeneo yao.
“Ni wajibu wetu sisi kama wataalamu wa mawasiliano kuhakikisha tunakuwa na mikakati amdhubuti ya mawasiliano katika Halmashauri zetu ili kufanyikisha utoaji wa taarifa kwa jamii juu ya namna ambavyo Serikali yetu inavyotekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo”, alisema Bibi. Zamaradi.
Aliongeza kuwa inasikitisha kuona baadhi ya Halmashauri nchini zinakosa kuwa na Maafisa Habari ambao wajibu wao ni kuhakikisha watanzania wanapata kujua nini Serikali yao inafanya katikati maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida Mhandisi Godfrey Sanga amesema kuwa habari ni suala muhimu sana katika ustawi wa jamii kutokana na ukweli kwamba bila mwananchi kupata taarifa juu ya nini Serikali yao inafanya wanakuwa kama wako gizani wakati ni ukweli kwamba yapo mengi ambayo Serikali yao inayafanya kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.
“Niseme tu kuwa kwa sasa habari ni kama uti wa mgongo, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha wananchi wanapata habari za uhakika tena kwa wakati, kwa kutambua hilo katika Halmashauri yetu tuaendeleo kuhakikisha wananchi wanapata habari na tutamuwezesha Afisa Habari wetu kadri ya mahitaji yake” alisema Mhandisi Sanga.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO), Bibi. Sarah Msika amesema kuwa TAGCO kwa kutambua jukumu kubwa walilonalo wanachama wake kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamekuja na mkakati wa kutembelea Maafisa wa Habari maeneo yao ya kazi ili kujionea namna wanavyofanya kazi na kushauriana nao namna bora ya kuongeza ufanisi katika kazi zao.
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na TAGCO wamekuwa katika ziara ya kutembelea Maafisa Habari katika maeneo yao ya kazi ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kilichofanyika machi 12 hadi 16 mwaka huu mkoani Arusha ambapo mpaka sasa wamekwisha tembelea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Ruvuma, Mtwara,Lindi, Tabora na Singida.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *