Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini

Kikao Kazi cha 15  cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Katibu Mwenezi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu kikao kazi cha 15 cha Maafisa Mawasilino Serikalini kitakachofanyika Mkoani Mwanza, Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Hicho Bi. Sarah Kibonde na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mwenezi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu kikao kazi cha 15 cha Maafisa Mawasilino Serikalini kitakachofanyika Mkoani Mwanza, Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Hicho Bi. Sarah Kibonde na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Ismail Ngayonga
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bi. Sarah Kibonde (katikati) akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu kikao kazi cha 15 cha Maafisa Mawasilino Serikalini kitakachofanyika Mkoani Mwanza, kushoto ni Katibu Mwenezi wa Chama hicho Dkt. Cosmas Mwaisobwa na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Ismail Ngayonga
DAR ES SALAAM, JUMANNE, 12 FEBRUARI, 2019 Wizara ya Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo, kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo na Chama cha Maafisa Habari Serikalini (TAGCO) wameandaa kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi, na Wakala wa Serikali (MDAs) kitakachofanyika Mkoani Mwanza kuanzia tarehe 18– 22 Machi 2018. Kikao kazi hiki kinachotarajiwa kuhudhuriwa na jumla ya Maofisa 300 ni cha 15 katika mfululizo wa vikao vinayofanyika kila mwaka kwa lengo la kuwajengea Washiriki uwezo wa namna ya kutangaza shughuli za Serikali. Aidha, kikao kazi hulenga pia kuziimarisha Idara/Vitengo vya Mawasiliano na Uhusiano Serikalini ili viweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Pia, Kikao Kazi, kinatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 18 Machi 2019 na kufungwa rasmi tarehe 22 Machi 2019 na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb). Aidha, katika Kikao Kazi cha 15, jumla ya mada 10 zitawasilishwa. Mada hizo zinalenga kujenga uwezo wa Maafisa kwenye masuala mbalimbali yahusuyo habari, mawasiliano, uhusiano na itifaki. Mada hizo zitawasilishwa na Wataalam watakaoleta uzoefu mpana katika mawasiliano. Pia, Kikao kazi kitatoa fursa ya kubadilishana uzoefu kati ya Maafisa Mawasiliano na wadau wengine wa habari. Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wanahimizwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 10 Machi, 2019. TAGCO ni chama kinachowaunganisha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano walioko Serikalini. Mkutano huu wa Maafisa Habari kwa mwaka huu, umedhaminiwa na: TANAPA, NCAA,  TANESCO, SHELL, SSRA, PSPTB,  na BOT. Imetolewa Na: SARAH KIBONDE MSIKA Makamu Mwenyekiti TAGCO

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos