Maafisa Habari Kuweni Vinara katika Kutangaza Habari za Serikali

Maafisa Habari Kuweni Vinara katika Kutangaza Habari za Serikali

Na Anitha Jonas & Shamimu Nyaki – WHUSM 02/12/2019, Dodoma. Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka Maafisa Habari nchini kuwa vinara katika kutangaza shughuli mbalimbali za serikali  ikiwemo miradi inayotekelezwa. Mhe.Shonza ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya awamu ya pili ya Maafisa Habari nchini

Na Anitha Jonas & Shamimu Nyaki – WHUSM

02/12/2019, Dodoma.

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amewataka Maafisa Habari nchini kuwa vinara katika kutangaza shughuli mbalimbali za serikali  ikiwemo miradi inayotekelezwa.

Mhe.Shonza ametoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya awamu ya pili ya Maafisa Habari nchini yanayofanyika kwa siku tano yenye lengo la kuwajengea uwezo.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akizungumza alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma.

‘Katika kutangaza habari za serikali kwa umma kila Afisa Habari ni lazima kutumia vyanzo vyote kusambaza habari ikiwemo mitandao ya kijamii kwa sababu inasambaza habari kwa haraka zaidi na kufikia watu wengi,’alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ufunguzi huo Naibu Waziri Shonza alisisitiza kuwa kwasasa waandishi wa habari  wanatakiwa kuwa na elimu kulingana na Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kwani tasnia hii inatakiwa kuondokana na makanjanja.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi awamau ya pili mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma..

Kwa Upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi amesisitiza kuwa Maafisa Habari wanapaswa kuandika na kutangaza habari za kimkakati zinazotekelezwa na serikali ili wananchi wafahamu maendeleo yanayofanywa na serikali.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kutangaza shughuli mbalimbali za serikali lakini wapo baadhi hawafanyi vizuri na ndiyo maana tumeona tuwape mafunzo haya ili kurekebishana katika utendaji,”alisema Dkt.Abbasi.

Naye Katibu wa Chama cha Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Abdul Njaidi amesihi Maafisa hao kuzingatia elimu watakayoipata katika mafunzo hayo ili waweze kutangaza vizuri utekelezaji wa Serikali katika maeneo yao.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi nakala ya Jarida Maalum la Nchi Yetu Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza mara baada ya ufunguzi rasmi wa awamu ya pili ya mafunzo ya Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari kutoka wizara, taasisi, mashirika ya umma na halmashauri nchini leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma. Jarida hilo ni toleo maalum linaloelezea mafanikio ya ndani ya Miaka Minne tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.Kulia ni Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi.

Pamoja na hayo mmoja wa Maafisa Habari Bibi.Nuru Mfaume kutoka  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda alitoa shukrani zake kwa Msemaji Mkuu wa Serikali na uongozi wa TAGCO kwa mafunzo hayo ambayo yatawaongezea ujuzi.

“Kweli kabisa mafunzo haya yametusaidia kujitathimini utendaji wetu na kugundua makosa yetu na baada ya hapa hakika kutakuwa na mabadiliko katika utendaji ikiwemo uandishi wa habari zetu”alisema Bibi.Nuru.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini mara baada ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mafunzo hayo leo tarehe 02 Desemba 2019 Jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi na Katibu wa Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw. Abdul Njaidi.

Mafunzo hayo yanahudhuriwa na Maafisa Habari mia moja kutoka Wizara,Taasisi,Mashirika,Mikoa na Halmashauri za Tanzania Bara ambapo mada mbalimbali zitatolewa.

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos