MAAFISA HABARI SERIKALINI WAAPA KUTOMWANGUSHA RAIS MAGUFULI

MAAFISA HABARI SERIKALINI WAAPA KUTOMWANGUSHA RAIS MAGUFULI

Na Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma   Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wameahidi kuitangaza miradi mbalimbali na kutomwangusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Wameyasema hayo leo (Ijumaa) wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano yaliyolenga kuwanoa katika kuandika kwa usahihi na umakini habari za Serikali.   Akifunga mafunzo

Na Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma
 
Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wameahidi kuitangaza miradi mbalimbali na kutomwangusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Wameyasema hayo leo (Ijumaa) wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano yaliyolenga kuwanoa katika kuandika kwa usahihi na umakini habari za Serikali.
 
Akifunga mafunzo hayo, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga, alimewataka maafisa hao kuitangaza miradi mbalimbali ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa wananchi.
 
“Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo makubwa sana ikiwemo ujenzi wa barabara za lami, madaraja, reli ya kisasa, ujenzi wa vituo vya afya na hospitali, utoaji wa elimu bila malipo, ununuzi wa ndege mpya pamoja na ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pale Dar es Salaam”.Amesema Mhandisi Nyamhanga.

 
Amesema, Maafisa Mawasiliano wanalo jukumu la kutangaza miradi hiyo na mingine mingi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Akifungua mafunzo hayo mapema wiki hii, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi aliwaeleza washiriki hao kuwa Rais Magufuli anataka kuona taasisi zote za umma zikitangaza kwa wakati na usahihi majumu waliyopewa kuyafanya.
 
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Afisa Habari wa Halmashauri ya Bahi, Dodoma, Bw. Benton Nollo amesema mafunzo hayo yamekuwa muhimu sana kwao na amemuahidi Rais Rais Magufuli kuwa hawatamwangusha na watatoka Dodoma wakiwa wameiva zaidi na wataboresha utendaji wao.
 
Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana naIdara ya Habari (MAELEZO).

Posts Carousel

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked with *

Latest Posts

Top Authors

Most Commented

Featured Videos