Kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini – TAGCO kwa pamoja imekubaliana kuwa Mkutano Mkuu wa Maafisa habari wa Serikali utafanyika Tarehe 09-13/03/2019 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya. Kamati hiyo imekutana tarehe 3/1/2020 kwenye Ofisi za TAGCO Jijini Dar ss salaam kwa kikao cha kawaida kujadili masuala mbalimbali ya
Kamati tendaji ya Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini – TAGCO kwa pamoja imekubaliana kuwa Mkutano Mkuu wa Maafisa habari wa Serikali utafanyika Tarehe 09-13/03/2019 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.
Kamati hiyo imekutana tarehe 3/1/2020 kwenye Ofisi za TAGCO Jijini Dar ss salaam kwa kikao cha kawaida kujadili masuala mbalimbali ya mustakabali wa chama hicho.
Akizungumza katika kikao hicho Katibu wa Tagco Abdul Njaidi amesema Mkutano huo umepangwa kufuatia ratiba ya kila mwaka na pia umezingatia maoni ya washiriki.
“Kikao cha mwaka huu kitakua cha tofauti kabisa na chenye manufaa zaidi kwa maafisa mawasiliano kwa sababu kimejikita katika kuleta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili maafisa hao katika maeneo yao ya kazi” amesema Njaidi.
Kikao hicho cha TAGCO kilipata baraka ya kuhudhuriwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dr. Hassan Abbas.
1 comment
1 Comment
Wazir Yakoub Wazir
January 5, 2020, 1:07 pmSafi sana viongozi wa Tagco kwa kuwajali Sana wanataaluma ya HABARI na mawasiliano serikalini nchini kwa kuwakutanisha pamoja Watumishi hapo kuelezea changamoto zao za kazi Na kuzitatua@ Karibuni KISARAWE Dc hapa kazi tu tunatekeleza ilaa ya CCM kwa vitendo 2020 CCM teba
REPLY