Na. Paschal Dotto-MAELEZO Kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kinatarajia kufanyika Machi 9-13, 2020 Jijini Mbeya ambapo Zaidi ya Maafisa 400 wanatarajia kuhudhuria Mkutano huo ambao utaangazia Zaidi katika kuangalia nini sekta hiyo muhimu imetekeleza katika azma ya kuisemea serikali kwenye kazi inazotekeleza kwa wananchi. Akizungumza katika Mkutano na Waandishi
Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kinatarajia kufanyika Machi 9-13, 2020 Jijini Mbeya ambapo Zaidi ya Maafisa 400 wanatarajia kuhudhuria Mkutano huo ambao utaangazia Zaidi katika kuangalia nini sekta hiyo muhimu imetekeleza katika azma ya kuisemea serikali kwenye kazi inazotekeleza kwa wananchi.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TAGCO Pascal Shelutete alisema kuwa kikao hicho kitalenga kuimarishha kada hiyo kwenye Taasisi za Serikali ili kuweza kutangaza mambo yanayofanywa na Serikali kwa wananachi.
“Kikao kazi hiki ni mwendelezo wa vikao vinayofanyika kila mwaka kwa lengo la kuwajengea Washiriki uwezo na pia kuimarisha Idara/Vitengo vya Mawasiliano na Uhusiano Serikalini katika kutangaza shughuli za Serikali hasa mafanikio katika utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano” alisema Shelutete.
Kikao hicho kinaratibiwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kinafanyika kwa mara ya 15 ambapo mwaka jana kilifanyika Machi 18 Jijini Mwanza.
Kikao hicho kitahusisha Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi, na Wakala wa Serikali (MDAs), pamoja na kutoka katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali ambapo washiriki watafanya tathmini ya utendaji kazi wao kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
TAGCO ilianzishwa rasmi mwaka 2012 na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria za Nchi, na inajumuisha watumishi wa umma wanaoshughulika na masuala ya Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki Serikalini.
prima cartoonize | numero de serie solidworks 2019 |
2 Comments
JhonEdison
August 19, 2024, 3:36 pmWhat are they doiing to our citixens? Someone tell me <a href="https://proappcrack.com/">here</a>
REPLYSoftHat
August 19, 2024, 3:45 pmThe TAGCO meeting focused on strategic growth, collaboration, innovation, and setting new goals for future success. Exciting prospects! Great action take by the government of Tanzania.
REPLY