TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Katibu Mwenezi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu kikao kazi cha 15 cha Maafisa Mawasilino Serikalini kitakachofanyika Mkoani Mwanza, Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Hicho Bi. Sarah Kibonde na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari-MAELEZO
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
DAR ES SALAAM,
JUMANNE, 12 FEBRUARI, 2019
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo na Chama cha Maafisa Habari
Serikalini (TAGCO) wameandaa kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano,
Uhusiano na Itifaki wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Taasisi, na Wakala wa
Serikali (MDAs) kitakachofanyika Mkoani Mwanza kuanzia tarehe 18– 22 Machi
2018.
Kikao kazi hiki kinachotarajiwa kuhudhuriwa na jumla ya
Maofisa 300 ni cha 15 katika mfululizo wa vikao vinayofanyika kila mwaka kwa
lengo la kuwajengea Washiriki uwezo wa namna ya kutangaza shughuli za Serikali.
Aidha, kikao kazi hulenga pia kuziimarisha Idara/Vitengo vya Mawasiliano na
Uhusiano Serikalini ili viweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Pia, Kikao Kazi, kinatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 18
Machi 2019 na kufungwa rasmi tarehe 22 Machi 2019 na Waziri wa Habari, Utamaduni
na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb).
Aidha, katika Kikao Kazi cha 15, jumla ya mada 10
zitawasilishwa. Mada hizo zinalenga kujenga uwezo wa Maafisa kwenye masuala
mbalimbali yahusuyo habari, mawasiliano, uhusiano na itifaki.
Mada hizo zitawasilishwa na Wataalam watakaoleta uzoefu
mpana katika mawasiliano. Pia, Kikao kazi kitatoa fursa ya kubadilishana uzoefu
kati ya Maafisa Mawasiliano na wadau wengine wa habari.
Maafisa Habari, Mawasiliano, Uhusiano na Itifaki wanahimizwa
kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 10 Machi, 2019.
TAGCO ni chama kinachowaunganisha Maafisa Habari,
Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano walioko Serikalini.
Mkutano huu wa Maafisa Habari kwa mwaka huu, umedhaminiwa
na: TANAPA, NCAA, TANESCO, SHELL, SSRA, PSPTB, na BOT.
Imetolewa Na:
SARAH KIBONDE MSIKA
Makamu Mwenyekiti
TAGCO
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *