Frank Mvungi- MAELEZO Maafisa Habari Katika Mkoa wa Mtwara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma. Akizungumza na Ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO uliomtembelea ofisini kwake , Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Alfred Luanda amesema kuwa jukumu la
Frank Mvungi- MAELEZO
Maafisa Habari Katika Mkoa wa Mtwara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.
Akizungumza na Ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO uliomtembelea ofisini kwake , Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Alfred Luanda amesema kuwa jukumu la Maafisa Habari ni kuhakikisha kuwa masiliano kati ya Serikali na wananchi yanakuwa yakimkakati na yanayoendana na kasi ya Serikali katika kuwahudumia wananchi.
“ Baadhi ya Maafisa Habari wanajiweka nyuma na kusahau kuwa wanalo jukumu kubwa la kuuhabarisha umma kuhusu miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao hasa kwenye Mikoa na Halmashauri” Alisisitiza Luanda
Akifafanua amesema kuwa umuhimu wa Afisa habari unatokana na namna anavyotekeleza majukumu yake kwa weledi hasa katika suala la mawasiliano ya kimkakati.
Aidha, alipongeza kazi zinazofanywa na Idara ya Habari na chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma.
Kwa upande wake muwakilishi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo amesema kuwa kila Afisa Habari ana jukumu la kuisemea Serikali katika Mkoa au Halmashauri ili kuwapa wananchi fursa ya kuelewa mikakati ya na miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao na kuachana na kasumba ya kufanya kazi kwa mazoea.
Naye Kiongozi wa ujumbe huo Bi. Gaudensia Simwanza amesema kuwa kuna haja kwa maafisa habari kupanua wigo wa utoaji wa taarifa za miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa kutumia mitandao ya kijamii.
Aliongeza kuwa Lengo la chama cha maafisa habari na mawasiliano Serikalini ni kuwajengea uwezo katika kuisemea Serikali.
Ziara ya ujumbe wa chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katika Mkoa wa Mtwara , Lindi na Ruvuma inalenga kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya ujumbe huo Maafisa Habari, na Viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa Halmashuri za Mikoa hiyo.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *